Miaka kumi na tatu ya Moto wa uamsho tunamtaka Bwana na nguvu zake






Wanawake Watumishi wa wamchao wampendao Kristo

Kuhusu Idara ya wanawake

Idara ya Wanawake imeanzishwa kwa mujibu wa ibara ya 20 sehemu ya 7 ya katiba ya Tanzania Assemblies of God. Hivyo kutokana na msingi huo Idara ya WWK imeandaa taratibu na muongozo wa Idara ya WWK kwa msingi wa kuongoza na kusimamia shughuli zote za Idara hii.

wanawake

DHIMA

Kuwa na wanawake wa kanisa la TAG mbao ni jeshi halisi la Bwana Yesu, walio jaa nguvu za roho mtakatifu, wenye kasi yakueneza na kutegemeza injili ambao maisha yao na ya jamii inayowazunguka huwa bora kwa mjibu wa kanuni za kibiblia. Pia idara ya WWK ipo kwaajili ya kuwaunganisha wanawake wote wa kanisa la TAG kitaifa na kanisa la mahali pamoja kwa kuwakuza kiroho, kuwapandikiza maono na mzigo wa kutumika na kutoa mafundisho yatakayowawezesha wanawake katika kanisa ili kutimiza agizo kuu kwa kutenda na kutoa mali zao.

KUSUDI

  1. Kuiletea Nyumba baraka kwa kua mke bora katika familia
  2. Kuliletea kanisa baraka kwa kushiriki huduma zote zinazohusu kanisa la mahali pamoja na kutoa fungu la kumi na michango yote ya kanisa kwa Uaminifu.
  3. Kumletea mchungaji na familia yake baraka kwa kumuombea mchungaji na familia yake pamoja na kuwasaidia katika mahitaji mengine.
  4. Kukiletea kijiji/mtaa baraka kwa kushiriki huduma zute za kijamii na kuonesha upendo wa kweli kimaneno na matendo.

MAADILI

  1. Uaminifu kwa Biblia kwa kuishi mafundisho yake.
  2. Kuwajibika kijamii tukidhihirisha upendo na Haki ya Mungu katika maneno na matendo.
  3. Kufanya pamoja kama timu kwa kua na mahusiaono mema baina yetu na watu wengine.
  4. Kuvuna Kimkakati.
  5. Kuwawezesha viongozi.
  6. Kukua kimkakati.
  7. Utawala wa fedha unaowajibika.