UWEZO FINANCIAL SERVICES
Tunakusikiliza, Unafanikiwa
Uwezo Financial Services Limited (UFSL) ni taasisi inayomilikiwa na kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG). Kampuni ya Uwezo inatoa mikopo midogo midogo na ya kati kwa makanisa, Taasisi za Makanisa, idara za kanisa (WWK, CAS na CMF), Wachungaji na washirika.Kampuni ya Uwezo ina lengo la kuwawezesha watanzania kukabiliana na changamoto za kiuchumi na kifedha kwa kutoa mikopo ya riba nafuu kwa wateja wake nawengine.

Maono
Kua taasisi ya kitaifa inayoongoza kwa kutoa mikopo ya riba nafuu kwa wateja wake.
Dhamira
Kampuni ya Uwezo Financial Services itachangia kuwezesha maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa wateja wake kupitia teknolojia ya huduma za kifedha na masoko.
Aina za mikopo
- Mikopo kwa maendeleo ya Kanisa
- Mkopo binafsi
- Mikopo kwaajili ya bIashara zilizo sajiliwa (rasmi)
MKOPO KWA AJILI YA BIASHARA RASMI
- Dhamana ya mali isiyohamishika
- TIN namba
- Passport size mbili za mmiliki wa biashara
- Barua ya utambulisho kutoka kwa mchungaji wako
- Barua ya utambulisho kutoka serikali ya mtaa
- Ada ya mkopo Tsh. 20,000/=
- Gharama za mchakato wa mkopo 2%
- Gharama za bima
- Gharama ya mwanasheria Tsh. 20,000/=
- Barua ya mkopo itaje dhumuni la mkopo, kiwango na muda utakaorejesha
- Kumbukumbu ya biashara angalau kwa miezi 6 ya hivi karibuni
- Taarifa za hesabu za Benki
- Barua ya mwenza wako kukubaliana na wewe kukopa isainiwe na mwanasheria na picha zake mbili
- Muda wa mkopo ni hadi miezi 24
MIKOPO BINAFSI
- Dhamana ya mali isiyohamishika
- Risiti za mafungu ya kumi angalau kwa miezi sita ya hivi karibuni
- Passport size mbili za muombaji wa mkopo
- Barua ya utambulisho kutoka kwa mchungaji wako
- Barua ya utambulisho kutoka serikali ya mtaa
- Ada ya mkopo Tsh. 10,000/=
- Gharama za mchakato wa mkopo 2%
- Gharama za bima
- Gharama ya mwanasheria Tsh. 20,000/=
- Barua ya mkopo itaje dhumuni la mkopo, kiwango na muda utakaorejesha
- Kumbukumbu ya biashara angalau kwa miezi 6 ya hivi karibuni
- Salary slip ya mwombaji wa mkopo za miezi 3 ya hivi karibuni
- Nakala ya Cheti cha ndoa
- Muda wa mkopo ni hadi miezi 24
MKOPO KWA MAENDELEO YA KANISA
- Dhamana ya mali isiyohamishika
- Muhtasari wa kikao cha baraza la kanisa
- Barua ya mtoa dhamana ithibitishwe na mwanasheria
- Taarifa ya mapato na matumizi ya kanisa kwa angalau miezi 6 ya hivi karibuni
- Hesabu za kanisa(Audit report) angalau kwa mwaka mmoja kwa mkopo onaozidi milioni 50
- Ripoti ya tathmini ya thamani ya jengo la dhamana kwa mkopo unaozidi milioni 20
- Barua ya utambulisho toka section
- Passort size mbili za mchungaji kongozi, mzee kiongozi na katibu wa kanisa
- Risiti za mafungu ya kumi ya kanisa kwa angalau miezi 6 ya hivi karibuni
- Ada ya mkopo nio Tsh50000/=
- Gharama ya mkopo 2%
- Gharama ya mwanasheria Tsh. 20,000/=
- Muda wa mkopo ni hadi miezi 24