SEHEMU
Kuhusu Sehemu
Ili kuleta ufanisi katika utekelezaji wa maono, malengo na majukumu mengine ya kanisa kama yalivyoainishwa, TAG itagawanywa kijiografia katika Sehemu.

Ili kuleta ufanisi katika utekelezaji wa maono, malengo na majukumu mengine ya kanisa kama yalivyoainishwa, TAG itagawanywa kijiografia katika Sehemu.
Kila Sehemu itamchagua Mwangalizi, Makamu Mwangalizi, Katibu na Mtunza Hazina. Uchaguzi wa viongozi wa Sehemu utafanyika mwaka unaofuata baada ya uchaguzi wa Baraza Kuu wakati wa konferensi za majimbo. Viongozi watakaochaguliwa watafanya kazi zao kwa muda wa miaka minne na uwezekano wa kuchaguliwa tena na tena.
Sehemu ambayo ina makanisa chini ya sita itaitwa sehemu inayoendelea. Kamati ya Jimbo itasimamia kama Waangalizi wa Sehemu hiyo. Kamati ya Jimbo inaweza kuteua mmoja wa watumishi katika Sehemu hiyo kuwa mwakilishi wao ambaye hatakuwa na haki ya kupiga kura kwenye Baraza la Waangalizi. Makanisa ya Sehemu hii yakiisha kukomaa Sehemu hiyo itatambuliwa kama Sehemu yenye uwezo wa kuwachagua viongozi wake.
Mahali ambapo kuna tatizo kubwa la kiuongozi ktika Sehemu, Kamati ya Jimbo itakuwa na mamlaka ya kupendekeza viongozi wa Sehemu kwa Kamati Kuu ya Utendaji. Uchaguzi wa sehemu utaendeshwa na Askofu wa Jimbo au mwakilishi wake aliyechaguliwa kutoka katika Kamati ya Jimbo. Wenye haki ya kupiga kura kuchagua viongozi wa Sehemu ni watumishi wote walio na makanisa na wenye vyeti vinavyotambuliwa na TAG.
Kwa maelezo zaidi Nunua katiba yetu sasa, Ili kununua
Uamsho ni Ajenda yetu.
Saa ya Uamsho ni Sasa.