MISINGI YETU YA IMANI

Tunaamini kwa dhati kuwa Biblia ndio Mwongozo wa imani yetu na matendo katika maisha yetu ya Kikristo. Tamko hili ndilo msingi wa ushirika wetu (1Kor.1:10; Mdo.2:42). Ukiri wa Imani yetu umejengwa katika misingi kumi na sita (16) ifuatayo:

Maandiko yaliyovuviwa

Tunaamni kwamba Maandiko yote ya Agano la kale na yale ya Agano Jipya yamevuviwa kihalisi na MUNGU na ni Ufunuowa MUNGU kwa wanadamu, ni mamlaka ya mwisho ya imani (2Tim 3:15-17, 1The 2:13, 2Pet 1:2).

MUNGU mmoja aliye Hai na wa kweli

Tunaamini kwamba MUNGU mmoja tu aliye hai na wa kweli ambae amekwisha kujunua mwenyewe kama 'MIMI NIKO' wa milele, muumbaji wa Mbingu na nchi na na mkombozi wa ulimwengu na wanadmu.(kumb 6:4, Isa 43:20-11).

Uungu wa Bwana Yesu

Tunaamini kwamba Bwana Yesu Kristo ni mwana wa MUNGU na anasifa zote za uungu (Yoh 1:1, lk 1:31-35, Mt 1:23).

Anguko la Mwanadamu

Tunaamini kwamba Mwanadamu aliumbwa kwa mfano wa MUNGU akiwa mzuri na mwema maana MUN GU alisema 'Na tumfanye mtu kwa mfano wetu na sura yetu' hata hivyo Mwanadamu kwa uasi wa hiari yake mwenyewe alianguka na kwa njia hiyo akajiletea mauti suo ya kimwili tu bali hata ya kiroho ambayo ni kutengwa mbali na MUNGU (Mwa 1:26-27; 2:17).

Wokovu wa Mwanadamu

Tunaamini kua tumaini pekee la ukombozi wa Mwanadamu ni kwa njia ya damu ya Yesu Kristo Mwana wa MUNGU iliyomwagika.(Luk 24:47 yohana 3:3).

Maagizo ya Kanisa

Tunaamini juu ya agizo la ubatizo wa kuzamisha linalotolewa na maandiko (Mt 28:19, Rum 6:4) Pia tunaamini juu ya meza ya Bwana mbayo ina mkate na matunda ya zabibu ni mfano wa kuelezea ushirika wetu wa asili ya Ki-MUNGU (2pet 1:4, 1Kor 11:26).

Ubatizo wa Roho Mtakatifu

Tunaamini kwamba waamini wote wanatakiwa na wanahaki ya kutafuta ahadi ya Baba yaani ubatizo wa Roho Mtakatifu (Luk 26:46, 1Kor 12:1-36).

Ushahidi wa Ubatizo katika Roho Mtakatifu

Tunaamini kwamba ubatizo wa waamini katika Roho Mtakatifu unashuhudiwa kwa ishara ya nje iliyo ya Kimwili ya kunena kwa lugha nyingine kwa Roho wa Mungu anavyowajalia (1Kor 12:4-10, 28).

Utakaso

Tunaamini kua utakaso ni tendo la kutengwa na kile kilicho kiovu na kujiweka wakfu kwaajili ya MUNGU (Rum 12:1-2, Ebr 13:12).

Kanisa

Tunaamini kwamba kanisa ni Mwili wa Kristo, Makao ya MUNGU kwa njia ya Roho, lenye vyeo vya Ki-MUNGU kwa ajili ya utimizo Kazi yake kuu (Efe 1:22-23, 2:22. Ebr 12:23).

Huduma

Tunaamini kwamba huduma ya ki-Mungu pamoja na utumishi uliopangwa na maandiko umetolewa na Bwana wetu kwa makusudi matano: (Mk 16:15, Efe.4:11-13, Yh.4:23-24, 1Kor.12; Rum.12, Mdo.2:42-46).

Uponyaji wa Kimungu

Tunaamini kwamba uponyaji wa kimungu ni sehemu muhimu ya Injili. Kufunguliwa kutoka magonjwa na vifungo mbalimbali ni haki ya kila anayeamini (Isa. 53:4; 5;Mt.: 8:16;17; Yak. 5:14-16).

Tumaini lenye Baraka

Tunaamini juu ya ufufuo wa wale ambao wamelala katika Kristo na kunyakuliwa kwao pamoja na wale waliohai waliosalia mpaka wakati wa kuja kwake Bwana ndilo tumaini lenye baraka na lililo kuu la Kanisa (1Thes.4:16, 17; Rum. 8:23; Tito 2:13; 1Kor.15:51, 52).

Utawala wa Kristo wa miaka Elfu

Tunaamini kuja kwa mara ya pili kwa Kristo ni pamoja na kunyakuliwa kwa Watakatifu ambalo ni tumaini lenye baraka, kukifuatiwa na kurudi kwa wazi kwa Kristo pamoja na Watakatifu wake kwa ajili ya kutawala hapa Ulimwenguni kwa muda wa miaka elfu moja (Zek. 14:5; Mt. 24:27;30; Ufu.1:7; 19;11-14; 20:1-6).

Hukumu ya Mwisho

Tunaamini kwamba kutakuwepo na hukumu ya mwisho ambayo humo wafu waovu watafufuliwa na kuhukumiwa sawa sawa na matendo yao. Yeyote ambaye hatakutwa ameandikwa katika Kitabu cha Uzima, pamoja na Shetani na malaika zake, mnyama na nabii wa uongo, watatupwa katika adhabu ya milele katika ziwa liwakalo moto na kibiriti, ambayo ni mauti ya pili (Mt. 25:46; Mk.9:43-48; Ufu. 19:20;20:11-15; 21:8).

Mbingu Mpya na Nchi Mpya

Kulingana na ahadi yake, tunatazamia mbingu mpya na nchi mpya ambamo haki yakaa ndani yake (2Pet.3:13; Ufu. 21 na 22).

Ili kupata nakala hii