Miaka kumi na tatu ya Moto wa uamsho tunamtaka Bwana na nguvu zake
Wanaume taifa kubwa la Watendakazi wa Wamchao Kristo.
Kuwepo kwa Idara hii kunahamasisha wanaushirika huu kufanya uamuzi wa dhati kuleta mabadiliko katika maisha yao na jamii yote.
Kuhusu Sisi
Idara ya Muziki na uimbaji kitaifa ilianzishwa rasmi mwezi septemba mwaka 2021. Kama kitengo cha muziki na uimbaji cha kusimamia mchakato wa uanzishwaji wa wa Idara hii wakati wa uongozi wa Askofu Mkuu wa TAG Dr.Rev. Barnabas Mtokambali. Uanzishwaji huu ulitoka na lengo mkakati (B4) la Miaka Kumi na tatu ya Moto wa Uamsho. Eneo la huduma ya Idara ya DMS litakuwa nchi yote ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Tanzania Bara na Zanzibar. Aidha, kwa mwongozo wa Ofisi Kuu ya TAG, idara hii itaweza kufanya kazi nje ya mipaka ya Tanzania. Jina la Idara ni “Idara ya Muziki na Uimbaji”, kwa Kiingereza “Department of Music and Singing” kwa kifupi “DMS”. Andiko la Idara ya DMS litakuwa ni Yohana 4:24 “Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.

MAONO
Maono ya DMS ni kuwa chombo cha kutafuta, kutunza na kuakisi Uwepo na Utukufu wa Mungu kupitia huduma ya Muziki na Ibada.
DHIMA
Idara ya DMS ipo ili kutunza uhai wa Kanisa kwa kuinua shauku na moyo wa Ibada iliyojaa madhihirisho ya nguvu za Roho Mtakatifu.
MAKUSUDI
Kufanyika “mkono” wa ofisi kuu, kamati za majimbo, kamati za Sehemu na uongozi wa Kanisa la mahali pamoja kuwafundisha washirika wa TAG kumwabudu Mungu katika uzuri (ubora) na utakatifu.