Miaka kumi na tatu ya Moto wa uamsho tunamtaka Bwana na nguvu zake
Ijue Idara ya Maombi TAG
Idara ya Maombi Kitaifa ilianzishwa Rasmi mwezi septemba mwaka 2021, wakati wa uongozi wa askofu Mkuu Dr. Rev. Barnabas Mtokambali, kutokana na Lengo Mkakati (A2) la Miaka 13 ya Moto wa Uamsho, Unatoa ufafanuzi kwamba idara ya Maombi imeanzishwa na Viongozi wa Idara wamepatikana. Lengo Kuu la Idara hii ni kuona kanisa lote tumeshika silaha hii kubwa ya Maombi ambayo ndio itakua Kichocheo kikubwa cha kusababisha uamsho wa kweli utokee.

MAONO
Kuwa kanisa la waombaji wasiokoma na kusababisha mlipuko na udhihirisho wa utendaji wa Roho Mtakatifu.
DHIMA
Kuandaa, kuratibu kusimamia na kuhamasisha maombi ili kulifanya kanisa kuwa waombaji wasiokoma.
MAKUSUDI
Kuhakikisha maombi ya kusababisha uamsho yanafanyika katika ngazi zote za kanisa na idara.
MAADILI YA MSINGI
- Uaminisu kwa Biblia
- Uadilifu
- Kuvuna kimkakati