Miaka kumi na tatu ya Moto wa uamsho tunamtaka Bwana na nguvu zake
Kuhusu Idara Yetu
Idara hii ilizaliwa rasmi mwaka 2008 na ikakabidhiwa kama ofisi rasmi na Mchungaji David mwakajinga tarehe 12/12/2008. Jambo hili lilikuwa ni utekelezaji wa matakwa ya katiba ya Tanzania Assemblies of God iliyokuwa imeagiza kuwepo na Idara hii. Vile vile Idara hii ilianzishwa kama chombo cha utekelezaji wa mpango mkakati wa kwanza wa kanisa chini ya Askofu mkuu mpya na wa awamu ya tatu ya maaskofu watanzania, Dktr, Barnabas Mtokambali. Viongozi waanzilishi walikua ni Rev. Elingarami Munisi aliyekua Mkurugenzi Mkuu, Rev, profesa Joseph Kimeme aliyekua Makamu wake, Rev. Moses Magembe aliyekuwa Katibu Mkuu wa Idara na huu ndio ukawa mwanzo wa Idara hii.
MAONO
Kuwa Idara inayofanya watu kuwa wanafunzi wa Yesu Kristo kitaifa na Kiulimwengu, waliojazwa na Roho Mtakatifu na wenye ushirika wa kiroho, Kufanya huduma inayoendana na mazingira na hivyo kulizidisha kanisa.
DHIMA
Kama Mkono wa TAG wa kutekeleza mpango mkakati, Idara hii itatimiza dira yake kwa kumjengea mshirika wa TAG msingi wa kuona maana ya kibiblia ya kumwabudu MUNGU. Pia ili mshirika aweze kukua kiibada, kihuduma, kiushirika na wenzake na kiutoaji chini ya uongozi na nguvu za Roho Mtakatifu.
MAADILI
|