Miaka kumi na tatu ya Moto wa uamsho tunamtaka Bwana na nguvu zake
Wanaume taifa kubwa la Watendakazi wa Wamchao Kristo.
Kuwepo kwa Idara hii kunahamasisha wanaushirika huu kufanya uamuzi wa dhati kuleta mabadiliko katika maisha yao na jamii yote.
Kuhusu Sisi
Maono ya kuwako kwa Ushirika wa Wanaume Wakristo, yaani Christian Men’s Fellowship (CMF) una historia ndefu katika TAG. Kwanza, wazo lilianza kama shauku ya uongozi wa Kanisa kitaifa, Pili, ilitokana na hitaji la wanaume wenyewe, na vilevile lilikuwa ombi la muda mrefu kutoka kwa Idara ya Wanawake Watumishi wa Kristo (W.W.K) wa kanisa letu. Mwaka 2008, wakati wa awamu ya tatu ya uongozi wa kanisa chini ya Askofu Dr. Barnabas Mtokambali, TAG ilitengeneza Dira ya Maendeleo ya Kanisa ya utekelezaji wa miaka kumi ya mavuno. Katika Eneo C linalosema “Inua viwango vya Ibada ya binafsi na pamoja”, kipengele cha C4:5-kina mkakati unaosema, “Anzisha Idara ya Wanaume”.

MAONO
Maono ya CMF ni kuona mwanamume aliyerejea katika nafasi yake ya awali ya uumbaji wa Mungu na kufanyika sifa na utukufu wa Kristo ili kutimiza kusudi la Kristo kupitia Kanisa pamoja na malengo ya TAG kitaifa.
DHIMA
CMF ipo ili kuwezesha wanaume kuabudu, kuwa na ushirika, kujengana, kutumika na kufanya uinjilisti.
DIRA
Kuwajenga na kuwaunganisha wanaume ambao ni washirika wa TAG ili kukuza umoja na ushirika miongoni mwao na kati yao na Kanisa (Mdo 2:44-47), Kujifunza kanuni mbalimbali za ki-Mungu za kufanikiwa kiroho na kimaisha ili kuwa kielelezo kizuri katika familia na jamii.