Miaka kumi na tatu ya Moto wa uamsho tunamtaka Bwana na nguvu zake
Idara ya Watoto na Wanafunzi ni Idara ndani ya kanisa la TAG, lilianzishwa rasmi Mwaka 1994 kufuatia mkutano wa viongozi wa Kanisa la Assemblies of God, barani Afrika, “Africa Assemblies of God Alliance” (AAGA) uliofanyika Nairobi, nchini Kenya mwaka mwaka 1993. Idara hii ilianzishwa ikiwa ni utekelezaji wa maazimio muhimu katika mkutano huo wa (AAGA). Mwaka huo wa 1994 kanisa la TAG lilikuwa linaongozwa na Askofu Mkuu Rev. Ranwell Mwenisongole na alimteua marehemu Mchungaji Joseph Justine kuwa Mkurugenzi Mkuu. Kadhalika, marehemu Mchungaji Jeremiah Kimaro aliteuliwa kuwa Makamu Mkurugenzi Mkuu na Mch. Everhard Mloka kuwa Katibu Mkuu. Huo ndio ukawa mwanzo mzuri wa Idara hii.
Bofya hapa kutembelea tovuti yetuKuwafanya watoto wa Tanzania kuwa wanafunzi wa Yesu Kristo, waliojazwa Roho Mtakatifu na kuukulia Wokovu, hatimaye wawe watumishi bora wa Bwana Yesu Kristo katika Kanisa lake.
Idara ya watoto ipo ili Kumhubiri Kristokwa watoto wa Tanzania, mashuleni, mitaani, majumbani, Kanisani na kuwafanya wanafunzi wa Yesu Kristo.
Askofu mkuu wa TAG mnamo tarehe 28 mwezi wa pili aliapishwa Rasmi na kua Mwenyekiti wa CPCT.
Semina za ILI zinatarajiwa kuanza hivi karibuni hivyo basi viongozi na wanachama wote wanaotakiwa kuhudhulia msipange kukosa.
Kwenye semina za uongozi za ili kutakua na Mafunzo pia kuhusu Mfumo wetu wa Bezaleli hivyo basi Kamati za Sehemu, Kamati za Idara Sehemu na Jimbo mnahimizwa kuhudhulia.
soma zaidiKutakua na Semina ya Uongozi ya ILI zitakazofanyika CCT, Morogoro hivyo basi Waalimu wa Vyuo Mama na Wenza Wao wanahimizwa kufika bila kukosa.
soma zaidiKutakua na kikao cha tathmini ya robo ya I ya mwaka kitakachofanyika Morogoro na wahusika wakuu ni Kamati ya Utendaji /Menejimenti
soma zaidi