Miaka kumi na tatu ya Moto wa uamsho tunamtaka Bwana na nguvu zake
Ijue Idara ya Vijana
Jina la Idara ni Tanzania Assemblies of God - Christ's Ambassadors (CA's); Yaani ikiwa na maana ya Vijana mabalozi wa Kristo.'Kimsingi ni Idara ya Vijana'.

MAONO
- 1: Walio jaa Roho mtakatifu kikamilifu.
- 2: Walio hamasika kihuduma.
- 3: Wenye mzigo na uwezo wa kuvuna roho zilizopotea kwa ufanisi mkubwa.
- 4: Kua na viongozi waaminifu na wawajibikaji katika ngazi zote.
DHIMA
- Kuhamasisha vijana.
- Kuunganisha Vijana.
- Kulea vijana katika malezi bora.
- Kupandikiza vijana Mzigo na Maono ya; -
- 1: Kuabudu kwa hiari yao baada ya kufundishwa umuhimu wa kumuabudu MUNGU.
- 2: Kutumika kwa bidii na viwango vya juu.
MAKUSUDI
- Kushuhudia.
- Idara inawaandaa vijana kwa mafunzo mbalimbali na kuwahamasisha ili kwa kutumia mbinu na njia mbalimbali waweze kufanya uinjilisti wenye Nguvu utawawezesha kuwaleta watu wenyedhambi kwa Yesu.